Your are here: Home // Habari // TEMEKE KUMEKUCHA SASA NI HOOLYWOOD YA BONGO!

TEMEKE KUMEKUCHA SASA NI HOOLYWOOD YA BONGO!

Wasanii wa Filamu Temeke

Wasanii wa Filamu Temeke wakiwa katika picha ya pamoja

TEMEKE KUMEKUCHA SASA NI HOOLYWOOD YA BONGO!

BAADA ya Wilaya ya Kinondoni kujenga umoja kwa wasanii wa filamu  Bongo, sasa Temeke wamekuja na kubwa kuliko mipango kama Hollywood vile, wasanii wanaotokea Wilaya ya Temeke wanaimarisha umoja wao na kuja kwa nguvu kubwa kwa kuwa na maadhimio makubwa katika ufanisi kiutendaji, wasanii hawa wameunda kamati ya kufanikisha matukio ,makubwa ikiwa utengenezaji wa filamu na tamthilia.

Salim Ahmed

Gabo zigamba mwigizaji wa Filamu Kiongozi wa Umoja Temeke

Mshindo Jumanne

Mshindo Jumanne mwigizaji wa Filamu Bongo

wasanii wa Filamu Temeke

Waigizaji nyota wakiwa katika picha ya pamoja Temeke

“Baada ya kukutana na kuamua jinsi ya kubororesha fani yetu, kila Jumamosi tunakutana na kutekeleza tuliyokubaliana, kwa kupitia kamati zetu hapa tupo katika mipango ya kufanya tamasha kubwa litakalowatambulisha wasanii wa Temeke,” alisema Mshindo Jumanne.

Umoja huo kwa kushirikiana na chama cha Waigizaji wa Temeke wanatarajia kuzindua filamu fupi ikiwa ni siku maalum kwa ajili ya kuwaunganisha wasanii wanaoishi Temeke, umoja huu unaoundwa chini ya Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ pia wapo wasanii Kama Fredy Sumari ‘Dile’, Mshindo Jumanne, Madebe Lidai, na wengine, ni siku ya Jumamosi nyingine kikazi zaidi wanakutana.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook