Your are here: Home // Habari // WASANII WA FILAMU TEMEKE KULAMBA DILI KUBWA – GABO

WASANII WA FILAMU TEMEKE KULAMBA DILI KUBWA – GABO

Salim Ahmed

Gabo Zigamba muigizaji wa Filamu Swsahilihood

MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amefunguka kuwa ni wakati wa wasanii wenye makazi na maisha yao, kulamba dume yaani kupata dili la kushiriki katika filamu fupi na baadae tamthilia, akiongea na FC mwenyekiti wa Sako kwa bako Gabo amesema kuwa ni muda muhimu sana kwa wasanii na wakazi wa Temeke kufaidika na vipaji vyao.

Athuman Mtindah

Ayhuman Mtindah mtayarishaji wa filamui na muongozaji wa filamiu

Salim Ahmed

Gabo akiwa katika pozi la picha

Salim Ahmed

Gabo Zigamba muigizaji mahiri wa Filamu Bongo.

Mshindo Jumanne

Mshindo Jumanne mjumbe Muongozaji wa filamu, Mtayarishaji,msambazajiMwanatemeke

Fredy Sumari

Viongozi wa chama cha waigizaji Temeke

Wasanii wa filamu temeke

Wasanii wanatemeke wakiwa katika kikao cha maandalizi

“Ni muda wa Wanatemeke kuibadili sura Temeke na kuwa alama ya tasnia ya filamu Tanzania, nawakaribisha wote kwa nia moja tu kuifanya Temeke kuendana na ukweli kuwa sehemu iliyobarikiwa na Mwenyezimungu kuzalisha vipaji hususani uigizaji, hivyo tarehe 03 na 04 mwezi wanane tujitokeze kwa wingi,”alisema Gabo Zigamba.

Chama cha waigizaji Mkoa wa Temeke chini ya umoja wa Sako kwa Bako wamekusudia kufanya tamasha kubwa sana huku lengo kuu ikiwa ni kuwaunganisha wasanii waishio Temeke na viunga vyake vyote, tukio hilo linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya TTC Chang’ombe tarehe 3/8/2019 kuanzia asubuhi, na wale watakaowahi watajihakikishia nafasi kulingana na uwezo wao katika uigizaji.

Kwa upande wa wasaili mwenyekiti wa Sako kwa Bako Team Gabo Zigamba amesema kuwa wamejipanga vema kwani wanazuoni kutoka Chuo Kikuu, Bagamoyo na taasisi husika na masuala ya filamu watakuwepo, kundi hili linaundwa na Athuman Mtindah, Mshindo Jumanne, Anna Dungo,Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’, Cathy Rupia na wasanii wengine wengi wenye majina katika tasnia ya filamu Bongo.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook