POLE ODAMA KWA KUMPOTEZA MAMA YAKE MDOGO.

Jennifer Kyaka

Odama msanii wa filamu Swahiliwood aliyefiwa na mama yake mdogo.

MWIGIZAJI na mtayarishaji mahiri wa filamu Swahiliwood Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefiwa na mama yake mdogo aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, taarifa za awali zimesema kuwa mama huyo alifariki leo hii asubuhi katika Hospitali hiyo.
(more…)

filed under: Habari

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WATANZANIA WOTE.

MV. Skagit

Waokoaji wakiwasaidia majeruhi wa ajali ya meli ya MV. Skagit.

KWA mara nyingine, Watanzania tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.
(more…)

filed under: Habari

ODAMA KUNUNUA SCRIPT ZA FILAMU MWAKANI.

Jennnifer Kyaka

Odama mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Jennifer Kyaka ‘Odama’ ameiambia FC kuwa kwa mwaka huu amesimamisha ununuaji wa muswada (Script) hadi mwakani mwezi wa kwanza ndio kampuni yake itaweza kununua miswada hiyo kutoka kwa watunzi na waandishi wa miswada hiyo katika kujipanga na kutoa ajira kwa wadau wa filamu.
(more…)

filed under: Habari

MPAMBANO WA KING MAJUTO Vs JB NI MOTO.

Jacob Stephen

JB Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI mahiri na mtayarishaji katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jacob Stephen ‘JB’ na gwiji la uchekeshaji Afrika Mashariki Amri Athuman ‘King Majuto’ wanakutana katika filamu ya Nakwenda kwa Mwanangu, filamu hiyo imetayarishwa na kampuni ya filamu ya Jerusalem ya jijini Dar es salaam.
(more…)

filed under: Habari

IVAN TEARS NA 69 RECORD ZAINGIA SOKONI.

Ivan-Tears- cut FC

Filamu ya Ivan Tears iliyoingia sokoni na kutikisa soko Swahiliwood.

FILAMU ya Ivan Tears kutoka Swahiliwood imeingia sokoni baada ya kufanyiwa uzinduzi katika ukumbi wa Maisha Club hivi karibuni, filamu hiyo kali na ya kusisimua ni moja kati ya filamu zinazosambazwa na kampuni ya Papa Zi Arts & Entertainment Promoters ya jijini Dar es Salaam, filamu ya Ivan Tears imeingia sokoni pamoja na 69 Record.
(more…)

filed under: Habari

MASANJA AFUNIKA IRINGA KATIKA UZINDUZI WAKE.

Emmanuel Mgaya

Masanja Mkandamizaji mchekeshaji mahiri Swahiliwood akitumbuiza jukwaani Iringa.

MCHEKESHAJI Mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Emanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ Jumapili iliyopita aliteka nyoyo za wapenzi wa muziki wa Injili kufuatia kufanya onyesho la kihistoria katika uwanja wa Samora Iringa, onyesho hilo lilikuwa ni la aina yake kufanyika mkoani Iringa na kujaza watu kila mtu aliyefika alifurahia Show hiyo.
(more…)

filed under: Habari

NAUNGA HARAKATI ZA BABA JANE MDOGO- RADO.

Simon Mwakipagata

Kapturado mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Simon Mwakipagata amesema kuwa ameamua kuendeleza harakati za msanii rafiki yake marehemu Steven Kanumba kwa kuwatumia watoto waliokuwa wakiigiza na msanii huyo alijizolea umaarufu zaidi baada kuibua vipaji vya watoto wadogo ambao walikuwa ni kivutio kwa wapenda filamu.
(more…)

filed under: Habari

NIMWIGIZE JOTI KWA KIPI- MASTER FACE .

Ali Juma

Master face mchekeshaji Swahiliwood kutoka kundi la Ze Comedy.

MSANII wa vichekesho Swahiliwood Ali Juma ‘Master face’ kutoka kundi la Ze Comedy ambalo urusha vichekesho vyake katika televisheni ya EATV amekanusha vikali kuwa yeye uhusika wake anamwiga sana msanii mwenzake kutoka kundi la Orijino komedi Joti kwa kila jambo analolifanya katika uigizaji wake katika kipindi cha Ze comedy.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU YA CHUNGU BORA ZIFF 2012.

FILAMU YA CHUNGU

Filamu ya Chungu iliyoshinda ZIFF tuzo kama Filamu Bora kutoka Swahiliwood.

ILE Filamu ya Chungu iliyorekodiwa katika Jiji la Tanga sehemu za Bumbuli imeibuka filamu bora katika tamasha la filamu Nchi za Majahazi Zanzibar International Film Festival (ZIFF), akiongea na FC mtayarishaji wa filamu hiyo ya Chungu kutoka Swahiliwood Dr. Vincensia Shule amesema kuwa ni faraja kwake na wadau wote wa filamu kwa kazi yao kuingia katika tamasha hilo na kushinda tuzo mbili.
(more…)

filed under: Habari

NAPIGA KAZI SIUZI SURA – MAC REAGAN .

Alex Chalamila

Mac Reagan Kipara mchekeshaji Swahiliwood akiwa moja ya kipande akirekodi na kundi la Orijino komedi.

MCHEKESHAJI Mahiri katika kundi la Komedi Orijino Alex Chalamila ‘Mack Reagan’ anasema katika kundi lao kila siku ni kazi, kwa hiyo inampasa kila msanii kuumiza kichwa kwa ajili ya kukaa juu bila kushuka kwani kundi lao ni kundi la kazi, lakini kwake anachojivunia ni kuwa na ubunifu wa kubuni maneno na kuwa maarufu mitaani lakini hata baadhi ya watu maarufu kuitumia kwake ni faraja.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook