BODI YA FILAMU IMELALA – MH.IDD AZAN.

Mh. Idd Azan

Mbunge wa Kinondoni Mh. Idd Azan mtetezi wa wasanii wa filamu Swahiliwood.

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azan ameishukia Bodi ya Ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza pale aliposema kuwa Bodi hiyo imelala kwa kushindwa kudhibiti na kukagua filamu kutoka nje, akichangia bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana Mh. Azan alisema kuwa anaona Wizara hiyo haina lolote inalofanya angependa ifutwe.
(more…)

filed under: Habari

KIWALO CHA JACK CHAVUTIA WAHEHE .

Jaqueline Wolper

Jack Wolper mwigizaji wa filamu Swahiliwood aliyetia fora kwa gauni lake Iringa hivi karibuni.

MWANADADA Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Masawe Wolper ‘Jack Wolper’ jumapili iliyopita alikuwa kivutia kwa wakazi wa Iringa baada ya gauni alilovaa kumpendeza na watu kushindwa kuamini kuwa aliyevaa alikuwa ni msanii ambaye pengine uonekana akiwa amevaa nguo za kutatanisha na kujiachia, lakini kwa siku hiyo alionekana kama mtawa au mwanamama mwenye familia yake asiye na makeke kabisa, tukio hilo lilitokea msanii huyo alipokuwa Mkoani Iringa katika uwanja wa Samora wakati wa uzinduzi wa muziki wa Injili kutoka kwa msanii Masanja Mkandamizaji.
(more…)

filed under: Habari

NGOZI YANGU KAZI YANGU VINANIPA DILI- AUNTY EZEKIEL.

Aunty Ezekiel

Aunty Ezekiel mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood balozi wa Zuku Swahili movie.

MSANII wa filamu na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Aunty Ezekiel amesema kuwa matokeo ya kuilinda ngozi yake kwa kutotumia vipodozi vikali na kujua ni aina gani ya vipodozi anavyostaili kutumia kwake imekuwa na faida kubwa sana, kwani kutokana na muonekano wa ngozi yake kuwa na mvuto inampata nafasi ya kufanya vizuri katika tasnia ya filamu lakini hata kupata matangazo na kazi nyingine katika tasnia ya filamu na sanaa kwa ujumla wake, msanii huyo aliyasema hayo baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa ZUKU.
(more…)

filed under: Habari

SITEGEMEI BUZI KATIKA KAZI ZANGU- ODAMA.

Jennifer Kyaka

Odama mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu.

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kwa kusema kuwa kazi zake za filamu anazotayarisha na kuweza kumudu kuendesha kampuni yake ya J- Film 4 Life Production haijatokana na fedha kutoka kwa mwanaume yoyote ambaye amewekeza kwake kwa sababu labda ana mahusiano naye, anasema kuwa yeye si mwanamke tegemezi kiasi ashindwa kutafuta fedha kwa ajili ya kuendesha mambo yake, binafsi anasema kuwa hapendi kutegemea wanaume kwani kwa kufanya hivyo hawezi kupiga hatua kimaendeleo.
(more…)

filed under: Habari

KESI YA LULU KUSIKILIZWA TENA AGOSTI 20 2012.

Elizabeth Michael

Lulu mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

KESI inayomkabili msanii wa filamu Swahiliwood, Elizabeth Michael maarufu ‘Lulu’, imeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, kutokana na Jaji anayeisikiliza kesi hiyo, DK Fauz Twaib kuwa na majukumu mengine.Akiahirisha kesi hiyo jana, Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, alisema Jaji Dk Twaib, anakabiliwa na majukumu mengine.
(more…)

filed under: Habari

KWANINI USHIRIKI WA WASANII ZIFF 2012 NI MDOGO?

Logo ziff 2012

Tamasha la filamu za majahazi (ZIFF 2012)

TAMASHA la 15 la filamu kwa nchi za Majahazi la Zanzibar International Film Festival (ZIFF), limemalizika hivi karibuni huku wasanii wengi wenye majina Swahiliwood wakishindwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo lenye hadhi kubwa Afrika ya Mashariki.
(more…)

filed under: Habari

DUME JEURI YA CHIKI KUIBUKIA GEITA.

Salum Mchome

Mwigizaji wa filamu Swahiliwood Chiki akiwa katika picha.

FILAMU kali na ya kusisimua kutoka Swahiliwood ya Dume jeuri imekamilika na ipo tayari kwa ajili ya kuingia sokoni baada ya kufanyiwa uzinduzi Kanda ya Ziwa sehemu itakayoonyeshwa filamu ya Dume Jeuri ni Geita na Kahama ,filamu hiyo imetayarishwa na Sharks T Ltd ya jijini Dar es Salaam akiongea na Chiki Mchoma ambaye ni mshiriki mkuu wa filamu hiyo amesema kuwa filamu itazinduliwa kanda ya Ziwa.
(more…)

filed under: Habari

POLE ODAMA KWA KUMPOTEZA MAMA YAKE MDOGO.

Jennifer Kyaka

Odama msanii wa filamu Swahiliwood aliyefiwa na mama yake mdogo.

MWIGIZAJI na mtayarishaji mahiri wa filamu Swahiliwood Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefiwa na mama yake mdogo aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, taarifa za awali zimesema kuwa mama huyo alifariki leo hii asubuhi katika Hospitali hiyo.
(more…)

filed under: Habari

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA WATANZANIA WOTE.

MV. Skagit

Waokoaji wakiwasaidia majeruhi wa ajali ya meli ya MV. Skagit.

KWA mara nyingine, Watanzania tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.
(more…)

filed under: Habari

ODAMA KUNUNUA SCRIPT ZA FILAMU MWAKANI.

Jennnifer Kyaka

Odama mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Jennifer Kyaka ‘Odama’ ameiambia FC kuwa kwa mwaka huu amesimamisha ununuaji wa muswada (Script) hadi mwakani mwezi wa kwanza ndio kampuni yake itaweza kununua miswada hiyo kutoka kwa watunzi na waandishi wa miswada hiyo katika kujipanga na kutoa ajira kwa wadau wa filamu.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook