TUWAOMBEE MZEE CHILO NA ZAWADI WAPONE HARAKA.

Ahmed Ulotu

Mzee Chilo msanii wa filamu Swahiliwood aliyelazwa KCMC Hospital.

WAPENZI wa tasnia ya filamu Swahiliwood wameombwa kuwaombea kwa sala wasanii mahiri na wenye mchango mkubwa katika tasnia hiyo ambao kwa sasa wapo katika maradhi yanayowasumbua na kulazwa Hospitali, wasanii hao ni Ahmed Uloto ‘Mzee Chilo, na Madina Hamis ‘zawadi’ wasanii hawa wamelazwa katika Hospitali tofauti tofauti.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU YA LAURA YAMTESA CHUCHU HANS .

Chuchu Hans

Chuchu Hans mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI mahiri wa filamu Swahiliwood Chuchu Hans amesema kuwa toka aanze kuigiza hajawahi kuigiza sehemu ngumu katika filamu kama aliyoigiza katika filamu ya Laura akiongea kwa unyonge alisema kuwa pamoja kuwa yeye ni binti wa Kiislamu lakini alilazimika kuingia katika sanduku la kuzikia akiwa kama mtu aliyefariki na kuagwa kwake ilikuwa ni mtihani.
(more…)

filed under: Habari

ALLY YAKUTI AMDHULUMU MKWANJA NANCY?!.

Godliver Godian

Nancy mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWANDISHI wa muswada Swahiliwood Ali Yakuti ameshutumiwa kwa kumdhulumu mwigizaji wa filamu hapa nchini Godliver Godian ‘Nancy’ malipo hayo yanatokana na ushiriki wa filamu ya Who is the Looser , filamu hiyo iliandaliwa na mwandishi huyo na kwenda kurekodiwa nje ya Jiji huko Kibaha, msanii huyo akiongea kwa uchungu amesema kuwa Yakuti ametumia nafasi ya kujuana kumdhulumu haki yake.
(more…)

filed under: Habari

BONGO MOVIE WACHANGISHANA KUMNUNUA MBOTO?.

HAJI SALUM

Mboto mchekeshaji Swahiliwood anayechangishiwa fedha kujiunga na Bongo Movie club.

MCHEKESHAJI Mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Salum Haji ‘Mboto’ amesema kuwa thamani yake ni kubwa kuliko fedha, msanii huyu amesema hayo wakati akiongea na FC, baada ya kuvuma uvumi kuwa wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Club wamefanya naye maongezi wakitaka ajiunge na kundi hilo lenye jina hapa mjini, lakini yeye akasema kuwa bado kwanza anajifikiria kuhusu jambo hilo.
(more…)

filed under: Habari

NIMERUDI SALAMA SASA KAZI TU- STARA.

Wastara Juma

Stara mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwoo.

MWIGIZAJI na mtayarishaji mahiri wa tasnia ya filamu Swahiliwood Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa anamshukru Mungu na Watanzania wote kwa ujumla baada ya kurudi salama kutoka nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu ya mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye pia ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.
(more…)

filed under: Habari

BIGGIE AINGIA FILAMU YA INJINIA KWA KISHINDO.

Lumole Motovolwa

Biggie msanii wa filamu Sawhiliwood anashiriki katika filamu ya Injinia.

MWIGIZAJI Mahiri wa filamu Swahiliwood mwenye muonekano wa kipeke Lumole Matovolwa ‘Biggie’ amefanikiwa kuchaguliwa kama ni mmoja kati ya wasanii wanaoshiriki kurekodi filamu ya Injinia filamu ya kipelelezi inayorekodiwa kwa kuwashirikisha wasanii wenye taaluma katika fani ya upelelezi, hadithi ya filamu ya Injinia ilihitaji kupata wahusika wenye uhalisia.
(more…)

filed under: Habari

BIDHAA ZA KANUMBA KUUZWA SABASABA.

Steven Kanumba

Marehemu Steven Kanumba gwiji la filamu Swahiliwood

FAMILIA ya msanii wa filamu Swahiliwood marehemu Steven Kanumba imeamua kuuza bidhaa za msanii huyo katika uwanja wa maonyesho wa Sabasaba uliopo Temeke, familia imefikia hatua hiyo katika kujenga utaratibu wa kumbukumbu kwa msanii huyo aliyekuwa nyota katika tasnia ya filamu Tanzania na kipenzi cha wapenda filamu filamu nchini.
(more…)

filed under: Habari

PAPA ZI YAINGIZA FILAMU NA KUTEKA SOKO.

Time after Time

Nyota wa filamu Swahiliwood Jack Wolper akiwa katika picha ya filamu ya Time after Time.

KAMPUNI ya Papa Zi Art & Entertainment Promoters inayoojishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa filamu Swahiliwood, katika kuhakikisha inanyanyua vipaji na kutangaza kazi zao imeingiza filamu kali na za kusisimua sokoni kwa mpigo, filamu hizo zikiwa sambamba na Onyesho la mkali wa muziki wa Bongo Fleva Nasseb Abdul ‘Diamond’ iliyopewa jina la Diamond are Forever iliyofanyika Mlimani City Live.
(more…)

filed under: Habari

NAPIGWA VITA KWA CHUKI- JACK WOLPER.

Jackqueline Wolper

Jack Wolper nyota wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper amefunguka kwa kusema kuwa kuna mtangazaji mmoja ambaye amekuwa akitumia nafasi yake kwa kumpiga vita na kumzushia kashifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujaribu kumtengenezea mazingira ya yeye kuingia katika ugomvi na wasanii wenzake wa kike, Jack amesema hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa gari yake aina BMw X 6 kuwa amenyeang,anywa.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU YA KOMANDO YOSO IMENISHUSHA- BIGGIE.

Lumole Matovolwa

Biggie msanii wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI wa filamu Swahiliwood Lumole Matovolwa ‘Biggie’ amekuwa tofauti na wasanii wengine ambao upenda kuelezea ni kazi gani ambayo kwake yeye imemvutia na kuikumbuka kila wakati wakati alipoigiza yeye anasema kuwa katika filamu zake
zote alizocheza hakuna filamu anayoichukia kama Komando yoso kazi ambayo hadi hataki hata kuiona.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook