ISIKE MTAYARISHAJI MKALI WA FILAMU.

Isike J. Samwel

Isike Mtayarishaji wa filamu mdogo mwenye kipaji Swahiliwood.

KAMA ni tuzo ya kupatiwa mtayarishaji mdogo kuliko wote na ana filamu nyingi zawadi hiyo ingekwenda moja kwa moja kwa Isike J. Samwel kijana mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Isike alianza kuandaa filamu yake ya kwanza kabisa akiwa katika umri wa chini ya miaka kumi nane wakati huo alikuwa kidato cha pili .
(more…)

filed under: Habari

MONALISA HANA HARAKA.

Yvonne Cherryl

Monalisa mtayarishaji na mwigizaji bora wa filamu Swahiliwood.

MWANADADA mahiri katika uigizaji tasnia ya filamu Swahiliwood Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ amesema kuwa anatumia muda mwingi kusoma soko la filamu na kupunguza kushiriki filamu kila mara jambo ambalo linamfanya aendelee kuwa bora kwa kipindi chote kwani wakati wasanii wengine wakishiriki filamu nyingi kwa mwaka lakini yeye ni agharabu kuigiza hata filamu tano kwa mwaka.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU PEKEE HAILIPI- KENNEDY.

Keneth Victor

Kennedy mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWINGIZAJI wa filamu Swahiliwood Keneth Victor ‘Kenned’ amesema kuwa kwa muda ambao amekuwepo katika tasnia ya filamu amegundua kuwa kutegemea sanaa ya uigizaji wa filamu pekee haulipi kwa maisha ya sasa, jambo ambalo angependa kuwashauri wasanii wenzake ni kujishughurisha na kazi nyingine au hata biashara kama anavyofanya yeye.
(more…)

filed under: Habari

HARUSI YA MTITU YAWAGAWA BONGO MOVIE NA TAFF.

William John Mtitu

Mtitu mtayarishaji na muongozaji wa filamu Swahiliwood bwana harusi mtarajiwa.

AWALI ilikuwa ukisema kuwa kuna mgawanyiko mkubwa katika tasnia ya filamu kwa wasanii hawa kuwa na vyama viwili vyenye sera tofauti, kila upande haukweka bayana hasa Bongo Movie Club, jambo hili linadhihirika leo siku ya Ijumaa asubuhi, kufuatia ujumbe ninaotumiwa na Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifwamba unaopiga marufuku msanii wa TAFF kudhuria kikao cha Harusi ya Mtitu Leaders .
(more…)

filed under: Habari

WASANII BILA SISI HAKUNA KITU- FARID UWEZO.

Farid Uwezo

Farid Uwezo mpiga picha na Mhariri wa filamu Swahiliwood.

MPIGA picha mahiri wa filamu Swahiliwood Farid Uwezo amejitamba kuwa wasanii bila ya wao wapiga picha hakuna msanii wa filamu ambaye anaweza kung’ra na kutamba katika tasnia ya filamu bila ya wao kuwapiga picha vizuri na wao kuonekana mbele za watazamaji kuwa nyota lakini wao watu wanaokaa nyuma ya kamera ikiwa ni pamoja na waongozaji wa filamu, wahariri wa filamu na watendaji wengine, filamu ni picha muongozaji na watu wengeni wanaokuwa nyuma ya kamera lakini anasema kuwa hakuna anayejua hilo ndio maana kuna watu wanaamua kuigiza.
(more…)

filed under: Habari

TUWAOMBEE MZEE CHILO NA ZAWADI WAPONE HARAKA.

Ahmed Ulotu

Mzee Chilo msanii wa filamu Swahiliwood aliyelazwa KCMC Hospital.

WAPENZI wa tasnia ya filamu Swahiliwood wameombwa kuwaombea kwa sala wasanii mahiri na wenye mchango mkubwa katika tasnia hiyo ambao kwa sasa wapo katika maradhi yanayowasumbua na kulazwa Hospitali, wasanii hao ni Ahmed Uloto ‘Mzee Chilo, na Madina Hamis ‘zawadi’ wasanii hawa wamelazwa katika Hospitali tofauti tofauti.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU YA LAURA YAMTESA CHUCHU HANS .

Chuchu Hans

Chuchu Hans mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI mahiri wa filamu Swahiliwood Chuchu Hans amesema kuwa toka aanze kuigiza hajawahi kuigiza sehemu ngumu katika filamu kama aliyoigiza katika filamu ya Laura akiongea kwa unyonge alisema kuwa pamoja kuwa yeye ni binti wa Kiislamu lakini alilazimika kuingia katika sanduku la kuzikia akiwa kama mtu aliyefariki na kuagwa kwake ilikuwa ni mtihani.
(more…)

filed under: Habari

ALLY YAKUTI AMDHULUMU MKWANJA NANCY?!.

Godliver Godian

Nancy mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWANDISHI wa muswada Swahiliwood Ali Yakuti ameshutumiwa kwa kumdhulumu mwigizaji wa filamu hapa nchini Godliver Godian ‘Nancy’ malipo hayo yanatokana na ushiriki wa filamu ya Who is the Looser , filamu hiyo iliandaliwa na mwandishi huyo na kwenda kurekodiwa nje ya Jiji huko Kibaha, msanii huyo akiongea kwa uchungu amesema kuwa Yakuti ametumia nafasi ya kujuana kumdhulumu haki yake.
(more…)

filed under: Habari

BONGO MOVIE WACHANGISHANA KUMNUNUA MBOTO?.

HAJI SALUM

Mboto mchekeshaji Swahiliwood anayechangishiwa fedha kujiunga na Bongo Movie club.

MCHEKESHAJI Mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Salum Haji ‘Mboto’ amesema kuwa thamani yake ni kubwa kuliko fedha, msanii huyu amesema hayo wakati akiongea na FC, baada ya kuvuma uvumi kuwa wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Club wamefanya naye maongezi wakitaka ajiunge na kundi hilo lenye jina hapa mjini, lakini yeye akasema kuwa bado kwanza anajifikiria kuhusu jambo hilo.
(more…)

filed under: Habari

NIMERUDI SALAMA SASA KAZI TU- STARA.

Wastara Juma

Stara mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwoo.

MWIGIZAJI na mtayarishaji mahiri wa tasnia ya filamu Swahiliwood Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa anamshukru Mungu na Watanzania wote kwa ujumla baada ya kurudi salama kutoka nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu ya mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye pia ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook