RICHIE KUZINDUA FILAMU YAKE MERERANI.

Jaqueline Wolper, Single Mtambalike, Adam Kuambina

Picha za wasanii wa Filamu ya Chaguo langu kutoka Swahiliwood.

BAADA ya uzinduzi wa filamu ya Toba ya mwigizaji mahiri wa filamu Swahiliwood Issa Mussa ‘Cloud 112, kufanyika kwa mafanikio huko Zanzibar na kukusanya wapenzi wa tasnia ya filamu zoezi hilo limevutia watayarishaji wengine, sasa ni zamu ya msanii mkongwe katika tasnia ya filamu na maigizo Swahiliwood Single Mtambalike aka Richie richie anazindua filamu yake ya Chaguo langu huko Mererani.
(more…)

filed under: Habari

AISHA KAMBONGO ATIKISA KIDUCHU FILMS.

Aisha Kambongo

Aisha Kambongo msanii chipukizi Swahiliwood.

KATIKA Usaili wa kutafuta wasanii wenye vipaji watakaoshiriki katika filamu fupi fupi zinajulikana kama Kiduchu Films kazi inayoandaliwa na kampuni ya A TOK ya jijini Dar es Salaam, kulikuwa na mambo ya kufurahisha sana kutoka kwa wasanii au washiriki waliofika katika tukio hilo, lakini pia kuna wasanii walikuwa kivutio KWA HABARI ZAIDI NA PICHA INGIA NDANI….
(more…)

filed under: Habari

FILAMU KUBWA YA CPU NDANI YA ZIFF 2012.

Juma Nkwabi, Subira Wahure, Sauda Simba, Steven Sandhu

Wasanii waliocheza filamu kubwa ya CPU Swahiliwood katika picha.

FILAMU Kubwa kutengenezwa Swahiliwood na vijana wa kizalendo ya CPU imechaguliwa kuwa ni mojaya filamu zitakazoonyeshwa na kushindanishwa katika tamasha kubwa la filamu la Zanzibar International Film Festival (ZIFF), filamu ya CPU ni filamu ya kipekee iliyotengenezwana Kampuni ya Haak Neel Production kwa ushirikiano na kampuni ya Wegos Works Ltd zote za jijini Dar es Salaam.
(more…)

filed under: Habari

JACK WOLPER AWAPAGAWISHA WANAFUNZI BARACKS.

Jaqueline Wolper

Jack Wolper nyota wa filamu Swahiliwood.

KATIKA hali ya kushangazwa na kuonyesha jinsi gani mwanadada nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Jacqueline Wolper ni kivutio, wanafunzi wa shule ya msingi Baracks ilipo maeneo ya Kilwa Road walitimkia nje kwa ajili ya kwenda kumwona Jack huku wengine wakimrukia mwilini mwake na kumfanya awe katika wakati mgumu hadi Polisi walipokuja na kuwaamuru wanafunzi hawa kurudi madarani walikokuwa wamewakimbia walimu wao.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU YA LAP TOP IMENING’ARISHA- HALIMA ALI.

Halima Ali

Msanii wa filamu Ritha binti anayetikisa Swahiliwood kwa filamu ya Lap Top.

MWIGIZAJI wa filamu chipukizi wa Swahiliwood Halima Ali amesema kuwa yeye hayupo single kama watu wanavyofikiria na kutumia muda mwingi kumsumbua wakijua ni binti mdogo ambaye pengine anahitaji kuwa na mahusiano na mtu mwingine, yeye hahitaji mpenzi kwani tayari ana mchumba na hayupo huru kwa ajili ya mtu mwingine, anasema usumbufu ameanza kuupata baada ya filamu ya Lap Top kutoka KWA HABARI NA PICHA ENDELEA NDANI…
(more…)

filed under: Habari

FILAMU INAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA- UNCLE CHRISS.

Chrissant Mhenga

Uncle Chriss Muongozaji na mtayarishaji wa filamu na tamthilia Swahiliwood.

MUONGOZAJI wa filamu na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Chrissent Mhenga ‘Uncle Chriss’ amesema kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa ili ilete tija na maslahi kwa watayarishaji na wasanii kwa ujumla, Chriss ameyasema hayo wakati akijiandaa kuandaa filamu mpya inayotarajia kuwashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Chriss ambaye ndiye mwasisi wa kizazi kinachotamba katika filamu ameamua kuingia rasmi katika filamu.
(more…)

filed under: Habari

KUHARIRI FILAMU NI KAZI NGUMU- MANGUSHI.

Said Abdalah Mangushi.

Mangushi Mhariri wa filamu na video za muziki wa taarab Swahiliwood.

MHARIRI mahairi wa filamu Swahiliwood Said Abdalah Mangushi ‘Mangushi’ anasema kuwa kazi ya uhariri wa filamu ni ngumu sana hasa pale unapokutana na wasanii wakubwa katika kuhariri filamu zao, akiongea Mangushi ameleza kuwa wasanii wengi hasa
wakubwa wana matatizo ya muda na wasumbufu katika ushauri jambo linalomfanya afikirie kufanya kazi na wasanii chipukizi.
(more…)

filed under: Habari

NAWASHUKRU KWA KUNIPOKEA – MAMA RITHA.

Hamida Atosi

Hamida Atosi mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu Swahiliwood Hamida Atosi ‘Mama Ritha, amewashukru wapenzi wa filamu Tanzania kwa kumpongeza kutokana na filamu aliyoigiza ya Lap Top baada ya kutoka na kupokelewa vizuri kutokana na uigizaji wake wa kuvutia, filamu ya Lap Top imetayarishwa na Gallus Mpepo na kuandikwa na Octavian Natalis ‘Mdau’.
(more…)

filed under: Habari

HATUNA UONGOZI KATIKA FILAMU- DAVID

Eliya Mjatta

David Msanii wa filamu Swahiliwood asiyeamini kama kuna viongozi katika filamu.

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Eliya Mjata ‘David Senior’ amewashukia wasanii wenzake kwa kukosa umoja na kujikomboa katika kusimamia maslahi yao ambayo kila siku imekuwa tatizo kubwa kwa wasanii na watayarishaji, pamoja na hayo pia amewalaumu viongozi wa makundi mawili yaani Bongo movie na Taff kwa kutumia muda mwingi kuongelea mambo binafsi kuliko maslahi ya wasanii kwa ujumla.
(more…)

filed under: Habari

USAILI FILAMU YA INJINIA MOTO.

Jaqueline Wolper

Jack Wolper mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

FILAMU ya aina yake ya Injinia inayotarajia kuanza kutengenezwa kutoka Swahiliwood imeingia katika hatua nyingine baada ya usaili wa kwanza kwenda vizuri kwa kuwapata wahusika watakaoshiriki katika filamu hiyo, filamu inayotabiriwa kuwa na mapinduzi makubwa kutokana na maandalizi yake huku suala la taaluma na nafasi kwa wahusika zikizingatiwa.

(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook