NKWABI JUMA AWAPA SHAVU WASANII CHIPUKIZI.

Nkwabi Juma

Nkwabi msanii wa filamu na tamthilia kutoka Swahiliwood.

MSANII wa filamu katika tasnia ya filamu Swahiliwood Nkwabi Juma Jumapili iliyopita alifanya usaili kwa kuchagua wasanii, watayarishaji, waongozaji wa filamu pamoja na wapiga picha wanaotarajia kushiriki katika filamu fupi fupi zitakazojulikana kwa jina la Kiduchu Films filamu hizo zitakuwa zikirushwa kupitia Televisheni ya Clouds Tv.
(more…)

filed under: Habari

KIPEMBA KURUDI KATIKA FILAMU.

Issa Kipemba

Kipemba msanii mahiri wa filamu Swahiliwood anakuja na filamu ya Injinia.

MWIGIZAJI na Mchekeshaji wa filamu Swahiliwood Issa Kipemba anarudi katika tasnia ya filamu kwa nguvu baada kukaa muda mrefu bila kurekodi wala kujishughulisha na kazi za filamu kwa muda mrefu, Kipemba anasema kuwa kwa muda huo alikuwa akifanya utafiti kuhusu filamu na sasa amepata jibu kwa ajili ya kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu hapa Swahiliwood.
(more…)

filed under: Habari

BARAFU KUJA NA FILAMU KALI YA LAURA.

Suleima Barafu

Barafu Mtayarishaji, Mwigizaji, na Muogozaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na Muongozaji wa filamu mahiri kutoka Swahiliwood Suleiman Said Abdallah ‘Barafu’ amejifungia kambini akirekodi filamu kali nay a kusisimua, akiongea kutoka mafichoni Barafu kasema kuwa baada ya kukamilika maandalizi na kuipitia vizuri muswada wa filamu yake hiyo mpya inayojulikana kwa jina la Laura, kazi ilikuwa kubwa sana kuwapata wasanii wanaoendana na hadithi hiyo.
(more…)

filed under: Habari

WEMA SEPETU NYOTA ING’ARISHAYO WASANII BONGO.

Wema Abraham Sepetu

Wema Sepetu msanii wa filamu Swahiliwood msanii mwenye mvuto mkali.

UNAPOONGELEA Wasanii wenye matukio na visa katika tasnia ya filamu Swahiliwood jina la Wema Sepetu si geni kwa kila mdau na mpenda sanaa kwa ujumla wake msanii huyu nyota yake ilianza kung’ara mwaka 2006 pale alipochaguliwa kama Miss Tanzania, hivi sasa mwanadada huyo amezidi kung’ara zaidi KWA HABARI NA PICHA ZAIDI ENDELEA……..
(more…)

filed under: Habari

ZAIDI YA WATU 500 WAJITOKEZA KATIKA KIDUCHU FILMS.

Wasanii walioshiriki Kiduchu films

Wasanii walioshiriki Kiduchu films

ZAIDI ya wasanii 500 wamejitokeza katika usaili kwa ajili ya kushiriki katika maandalizi ya filamu fupi fupi zitakazojulikana kwa jina la Kiduchu Films, usahili huo ulifanyika leo hii katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni na kuhudhuriwa na umati wa watu mbalimbali huku wote wakiwa na shauku ya kuibuka kama washindi watakaochaguliwa, akiongea na FC mratibu wa zoezi hilo Nkwabi Juma amesema. KWA MATUKIO NA PICHA ENDELEA NDANI…….
(more…)

filed under: Habari

ZIFF YATAFUTA WAFADHILI ZAIDI SLIPWAY HOTEL DAR.

ziff-logo

ZIFF mwaka 2012 kufanyika Julai 7- 15.

ZIFF imezindua shughuli ya kutafuta wafadhili wa tamasha kwa kufanya tafrija kwa wadau na wafadhili wake.Katika usiku wa wafadhili uliofanyika katika Hotel ya Slipway jana ZIFF inajishaua kwa maringo kwa kuweza kufanya matamasha 15 yenye mafanikio na ya sifa nchini na Afrika.
(more…)

filed under: Habari

MH. MAKALA ATOA RAMBIRAMBI KWA KANUMBA.

Frola Mtegoa

Mama wa masnii wa filamu Swahiliwood marehemu Kanumba.

SERIKALI imetekeleza ahadi iliyotoa wakati wa msiba wa gwiji la tasnia ya filamu Swahiliwood Marehemu Steven Kanumba, zoezi hilo lilifanyika nyumbani kwa marehemu Kanumba Sinza Vatcan City, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Amos Makalla aliwakilisha serikali kutoa rambirambi ya shilingi milioni 10, kwa familia ya Marehemu Kanumba.
(more…)

filed under: Habari

BONGO MOVIE WAPAMBA USIKU WA ZIFF.

Vincent Kigosi

Mtitu akiwa na JB katika pozi.Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja

Ray The Greatest Mtayarishaji na Muongozaji filamu Swahiliwood alikuwepo usiku wa ZIFF Slipway.

WASANII wa tasnia ya filamu kutoka Swahiliwood walipamba hafla ya ZIFF usiku wa jana siku ya Jumatano 30,Mei,2012 sherehe hizo zilifanyika katika Hotel ya Slipway na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali huku wengi wakiwa ni wasanii kutoka kundi la Bongo Movie Club chini ya Mwenyekiti wao Jacob Stephen ‘JB’ wasanii hawa waliingia katika ukumbi kila msanii kwa nyakati tofauti huku wakiwa wamependeza.

(more…)

filed under: Habari

STEVEN SANDHU KUWAANGALIA WAZEE.

Steven Sandhu

Steven Sandhu mwigizaji na mmiliki wa kampuni ya Triple S Entertainment.

MSANII Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Steven Sandhu amegeukia huduma za kijamii zaidi baada ya kufungua kampuni yake inayojulikana kwa jina la Triple S Entertainment, anasema kampuni hiyo pamoja itajihusisha na masuala ya filamu na burudani kwa ujumla lakini kazi ya kwanza ambayo kampuni hiyo inaanza nayo ni kusaidia Wazee wasiojiweza.
(more…)

filed under: Habari

SADIKINA MUSSA MPINZANI WA WEMA SEPETU.

Sadikina Mussa

Sadikina Mussa msanii chipukizi katika tasnia ya filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu Swahiliwood Sadikina Mussa anasema kuwa katika tasnia ya filamu hana mpinzani kabisa angalau kidogo mtu ambaye anaweza kwenda naye sambamba na kumfikia katika uigizaji kwa wasanii wa kike ni Wema Sepetu tu ndio anayemuona anaweza kushindana naye katika fani hiyo ya uigizaji.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook