SADIKINA MUSSA MPINZANI WA WEMA SEPETU.

Sadikina Mussa

Sadikina Mussa msanii chipukizi katika tasnia ya filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI Chipukizi katika tasnia ya filamu Swahiliwood Sadikina Mussa anasema kuwa katika tasnia ya filamu hana mpinzani kabisa angalau kidogo mtu ambaye anaweza kwenda naye sambamba na kumfikia katika uigizaji kwa wasanii wa kike ni Wema Sepetu tu ndio anayemuona anaweza kushindana naye katika fani hiyo ya uigizaji.
(more…)

filed under: Habari

LOVENESS ANALIA NA SHOGA YAKE KWA UMBEYA.

Loveness Watson

Love mwigizaji wa filamu Swahiliwood aliyeibiwa Mchumba.

MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Swahiliwood Loveness Watson ‘Love’ amemlalamikia shoga yake wa karibu kwa kumkatia buzi lake kamba baada ya kumfanyia vitina kwa kumpigia simu na kumweleza umbeya kuhusu kuwa na uhusiano na king’asiti aliyetajwa kwa jina moja la George Love amemtaja shoga yake kwa jina la Theopista Reverian ‘Dina’.
(more…)

filed under: Habari

FILAMU YA TAMAA YANGU KUTOKA ALHAMISI – KAPTURADO.

Simon Mwakipagata

Kapturado Mwigizaji na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood Simon Mwakipagata ‘Kapturado’ anatarajia kuingia sokoni na filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Tamaa Yangu filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni hivi wiki hii siku ya Alhamisi , akiongea na FC Kapturado amesema kuwa filamu ya Tamaa Yangu ni kali na ya kusisimua filamu hiyo inakuja baada ya I think I hate my Wife kufanya vizuri.
(more…)

filed under: Habari

UKWELI NI SUMU KWA WABABAISHAJI- DUDE

Kulwa Kikumba

Dude Mwigizaji na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na Muongozaji mahiri wa filamu Swahiliwood Kulwa Kikumba ‘Dude’amezidi kushangazwa na jinsi wasanii wa Bongo Movie wanavyokimbilia kutisha watu wanaosema ukweli kuhusu matukio ambayo yamekuwa yakifanywa na wasanii wanaounda kundi hilo, akiongelea suala hilo Dude anasema kuwa alichosema katika kipindi cha Take One ndio ukweli wenyewe.
(more…)

filed under: Habari

BLOOD HOUSE IMENIPA MCHUMBA- ALLEN.

Elia Daniel ,Anna Matee

Allen na Angel wanaotarajia kuoana wasanii kutoka Swahiliwood.

MWIGIZAJI Nyota anayekuja juu katika tasnia ya filamu Swahiliwood Elia Daniel ‘Allen’ anasema kuwa filamu yao mpya ya Blood House (Nyumba ya Damu) inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni kwake imeleta faida kubwa kutokana na kufanya kuweza kumpata mchumba ambaye ni Anna Matee aliyeigiza kama Angel, katika filamu hiyo Allen na Angel wameigiza kama mke na mume.
(more…)

filed under: Habari

MSHINDO NA PENINA NI BALAA KATIKA HARAKATI.

Jenifer Raymond Mshindo Jumanne

Msanii Penina akiwa na Mshindo Jumanne kutoka swahiliwood.

MSHINDO Jumanne, muigizaji na mtayarishaji wa filamu mwenye fani lukuki amekamilisha filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la HARAKATI, Mshindo ambaye miezi kadhaa iliyopita alinukuliwa kuwa hatoandaa filamu zake mwenyewe na badala yake atafanya kazi za kampuni fulani jana ameyakana maelezo yake hayo na kusema kuwa sasa atasimama na kampuni yake ya SSG DISTRIBUTORS tu.
(more…)

filed under: Habari

SERIKALI IJIFUNZE KWA KIFO CHA KANUMBA.

Flaviana Matata

Flaviana Matata mwanamitindo wa Kimataifa.

MWANAMITINDO Flaviana Matata ameishauri serikali ijifunze kutokana na kifo cha msanii mahiri katika tasnia ya filamu Swahiliwood Steven Charles Kanumba na kutambua umuhimu wa kazi za wasanii, jinsi kwa juhudi zao binafsi kulitangaza Taifa Flaviana anasema kuwa hakuna faida ya msanii kusifiwa baada ya kifo.
(more…)

filed under: Habari

EVANS BUKUKU NDANI YA NYUMBANI LOUNGE.

Evans Bukuku

Evans Bukuku Mchekeshaji mahiri Swahiliwood.

MCHEKESHAJI Mahiri katika tasnia ya Vichekesho Swahiliwood Evans Bukuku na kundi lake la Evans Bukuku’s Comedy Club chini ya kampuni ya Vuvuzela Entertainment siku ya Jumanne tarehe 29. May. 2012 wataangusha bonge la Show katika kiwanja tulivu cha nyumbani Nyumbani Lounge Namanga jirani na Best Bite mkurugenzi Bukuku anahabarisha FC.
(more…)

filed under: Habari

MZEE SMALL ALAZWA AMANA HOSP.

Said Wangamba

Mzee Small mwigizaji wa filamu na vichekesho Swahiliwood aliyelazwa Hospitali ya Amana,

GWIJI la Sanaa na mwigizaji filamu na vichekesho Swahiliwood Said Wangamba ‘Mzee Small’ amelazwa katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam Mzee Small alilazwa katika Hospitali hiyo baada ya kuugua ghafla akitokea safarini Jijini Mwanza alikokwenda kwa ajili ya kuelimisha kupitia sanaa kukomesha mauaji watu wenye matatizo ya ngozi Albino.
(more…)

filed under: Habari

AROBAINI YA BI. CHAIBA KOMBO KUFANYIKA JUMAPILI HII.

Bi. Chaiba Kombo

Bi. Chaiba Kombo Mwanaharakati na mwandishi wa muswada Swahiliwood.

FAMILIA ya Mwanaharakati na mwandishi mahiri wa muswada wa filamu Swahiliwood Bi Chaiba Kombo inawakaribisha jamaa ndugu wadau wote wa tasnia ya filamu katika Arobaini ya kumaliza msiba wa ndugu yao siku ya jumapili tarehe 27. May. 2012, shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika Kimara Kona kwa Mzee Masabo.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook