Bongo na Flava Inapatikana Bure Youtube

Sinema yenye mastaa kibao wa muziki wa kizazi kipya haswa wale hip hop ama rap sasa imewekwa bure katika mtandao wa youtube na watayarishaji wake. Wakiulizwa je ni kwanini sinema yao hawajaamua kuizua, (more…)

filed under: Habari

ANAYEUA FILAMU BONGO NI NANI? TOKA 40M HADI LAKI ..KADHAA?!

Uncle JJ film

Filamu ya Uncle JJ ya Kanumba

KILA siku zinavyosonga hali ya soko la filamu Bongo linazidi kuwa tete hakuna matumaini tena waliobaki kupigania soko hilo ni wasanii wa komedi na moja ya sababu kuu ni kutokana na kuuza kazi zao kwa bei ya chini na si kwa gharama nafuu, wale wasambazaji wakubwa hawachukui tena filamu kwani usambazaji wake umekwama.
(more…)

filed under: Habari

NILIIKOSA SUTI YA MJENGONI KIDOGO SANA- KINGWENDU

Rashid Mwishehe

Kingwendu muigizaji wa filamu Swahilihood.

MCHEKESHAJI Komedi Bongo Rashid M Mzange ‘Kingwendu’ ametoa kali ya mwaka pale aliposema kuwa mwaka 2015 aliingia kugombea Ubunge huku hamu yake kuu akitamani sana kuvaa suti na Tai kama mheshimiwa Mbunge, lakini anasema hajakata tamaa anjipanga tena uchaguzi ujao mwaka 2020 ataingia katika kinyang’anyiro.
(more…)

filed under: Habari

SOKO LA FILAMU BONGO NI PRESURE- ZERISH

Helena Luanda

Zerish muigizaji wa filamu Tanzania

MUIGIZAJI wa filamu Bongo Hellen Luanda ‘Zerish’ anadai kuwa msanii akiigiza tu si rahisi kujipatia maslahi hivyo ni kujiingiza katika utayarishaji wa filamu hapo ndio msanii anaweza kupata maslahi zaidi lakini kufanya hivyo kuna changamoto kubwa kwani baadhi ya wasambazaji ni wasumbufu ambao wanafanya kazi nje ya makubaliano.
(more…)

filed under: Habari

TUNAHITAJI KIZAZI KIPYA BONGO MOVIE- STEVE NYERERE

Steven Mengele

Steve Nyerere mwenyekiti wa Bongo Movie mstaafu

STEVEN Mengele ‘Steve Nyerere’ ameibua mjadala mpya baada ya kusema kuwa tasnia ya Bongo movie imeingia katika changamoto ya kudorora kutokana na wasanii kuwa wale wale kila siku na kuwazuia wasanii chipukizi kuingia katika na kupewa nafasi kama waigizaji wanaofanya vizuri katika ukuaji wa tasnia hiyo.
(more…)

filed under: Habari

ZAWADI ZAWADI FC TATU SOKONI WIKI HII KINARA BABU THE PERFECT MAN

Babu the Perfect

Filamu ya Babu The Perfect Man

SOKO la filamu kutoka Swahilihood linaendelea kupigania nafasi yake huku wadau na wauzaji wa sinema wakisema kuwa zile kazi za zamani bado zina nafasi kubwa sana katika soko hilo, inapotoka filamu mpya inasaidia kuuzwa kwa filamu za kitambo wiki hii filamu ambazo zimeendelea kufanya vizuri ni Jamila na Pete ya Ajabu ikisindikiza filamu mpya namba mbili na tatu.
(more…)

filed under: Habari

NAPIGA MSAMBA NIIGIZE NA ANGELINA JOLIE – EBITOKE

Anastanzia Exavery

Ebitoke mchekeshaji wa Komedi Swahilihood.

KOMEDIANI wa kike Bongo movie Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ amefunguka kwa kusema kuwa kila kunapokucha anaiangalia sana sanaa anayoifanya na kujaribu kuifanya impe maslahi zaidi kwa kuishi hivyo ameamua kuanza mazoezi zaidi ya viungo na mwili kwa ujumla wake akiwa na na ndoto za kuigiza na muigizaji Angelina Jolie wa Marekani.
(more…)

filed under: Habari

UZALENDO SI KUVAA TU VITO NA MAVAZI- GABO

Salim Ahmed

Gabo Zigamba muigizaji wa filamu Swahilihood.

MUIGIZAJI nyota Bongo Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ anaongelea Uzalendo haujengwi kwa mavazi na vito vya thamani na kuna wakati waafrika wanaamini kuwa wapo Huru lakini inasikitisha wale walio wengi hawajui maana hasa ya uzalendo wakiamini kuwa uzalendo utajengwa kwa misemo na harakati za kuzunguka kwa kutengeneza fedha.
(more…)

filed under: Habari

KOMEDI IMENIPAISHA BONGO MOVIE- JANNIFER

Jennifer Temu

Jennifer Temu muigizaji wa filamu Swahilihood.

MUIGIZAJI wa kike Bongo Movie Jennifer Temu anabainisha kuwa amekuwepo katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu na kushiriki katika sinema nyingi lakini hakuwa na jina kama alivyogeukia komedi na kuona mafanikio katika uigizaji akiwa ameshiriki filamu nyingi kuliko komedi.
(more…)

filed under: Habari

TUMEUA FILAMU ZETU TUTAIWEZA TAMTHILIA? – KITALE

Mussa Kitale

Kitale Mkude simba muigizaji wa filamu Swahilihood.

MUIGIZAJI na mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu Swahilihood Mussa Kitale ‘Mkude Simba’ amefunguka kwa kusema kuwa soko la Bongo movie lilikuwa juu sana lakini hivi karibuni imetokea songombingo soko la filamu kushuka na wasanii, kukimbilia kuigiza tamthilia badala ya filamu kwani soko limekwama na kusuasua.
(more…)

filed under: Habari
Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook